Rais wa Chad kuwania muhula wa tano

Deby Haki miliki ya picha
Image caption Rais Deby ameongoza Chad tangu 1990

Kiongozi wa Chad Idriss Deby ametangaza kwamba atawania urais kwa muhula wa tano katika uchaguzi mkuu mwezi Aprili.

Bw Deby amekuwa uongozini tangu 1990.

Amesema atarejesha mipaka kwenye mihula ya urais iwapo atachaguliwa tena, shirika la habari la Reuters linasema.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Aliingia madarakani kupitia mapinduzi ya serikali

Bw Deby alichukua uongozi kupitia mapinduzi ya serikali 1990 na baadaye akarejesha mfumo wa kufanyika kwa uchaguzi.

Alishinda uchaguzi wa karibuni zaidi 2011.

Wapinzani wake wanamtuhumu kuwa ni kiongozi wa kiimla na wanasema uchaguzi nchini humo huwa si wa huru na haki.

Haki miliki ya picha Buhari Office
Image caption Bw Deby na kiongozi wa Nigeria Muhammadu Buhari

Bw Deby, ni mshirika mkuu wa Ufaransa na amesaidia sana katika operesheni ya kijeshi ya kukabiliana na wanamgambo wa Kiislamu kanda hiyo.