Mabadiliko ya tabia nchi kuongeza urefu wa safari

Haki miliki ya picha PA
Image caption Safari za ndege kuwa ndefu kutokana na mabadiliko ya tabia nchi

Safari za ndege kutoka Uingereza kuelekea Marekani huenda zikachukua mda mrefu kutokana na mabadiliko ya tabia nchi,kulingana na utafiti mpya.

Mabadiliko ya hali ya hewa huongeza urefu wa mkondo wa ndege na kupunguza kasi ya ndege zinazoelekea nchini Marekani.

Huku ndege zinazoelekea mashariki kutoka Marekani zikiwa na kasi ,mzunguko wa mkondo wa safari za ndege huongezeka.

Image caption upepo

Wanasayansi hao kutoka chuo kikuu cha Reading wanaamini kwamba mabadiliko yataongeza hewa chafu ya mkaa, utumizi wa mafuta na kusababisha kupanda kwa nauli za ndege.

Utafiti huo umechapishwa katika jarida la mazingira la Environmental Research Letters.