Facebook yaonywa kuhusu udukuzi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption facebook

Facebook imepewa miezi mitatu kuacha kuwafuatilia watu ambao sio wanachama wake katika mtandao huo bila ya idhini yao nchini Ufaransa.

Mwaka ulopita, mtandao huo ulifanya mabadiliko kuhusu vile ambavyo watu wanautazama nchini Ubelgiji kufuatia agizo kama hilo kutoka kwa kamishna wa maswala ya faragha.

Bodi hiyo ya kulinda data pia ilitaka kuwekwa kwa nywila yenye herufi nane badala ya ile yenye herufi sita.

''Kulinda faragha ya raia wanaotumia mtandao huo, ndio jukumu letu kuu.Pia tunapanga kujadiliana na mamlaka ya ulinzi wa data ili kujibu wasiwasi wao,''alisema msemaji.

Mtandao huo humfuatilia kila mtu anayeutembelea, bila kujali iwapo mtu ni mwanachama,kupitia kuweka kuki zinazokusanya habari kuhusu mambo yanayoendelea katika mtandao huo.

Nchini Ubelgiji ,wageni wanaozuru mtandao huo kwa sasa ni sharti waingie kupitia login ili kuweza kuona ukurasa wowote.

Vilevile Kituo hicho cha kulinda data CNIL pia kimeambia kampuni hiyo kusitisha uhamishaji wa data hadi Marekani kwa kuwa makubaliano hayo ya kuzihifadhi mahali salama yamekwisha.

Facebook imesema kuwa inatumia mikataba mingine ya kisheria kuhamisha data yake hadi nchini Marekani.

Makubaliano hayo ambayo yaliwezesha usafirishaji wa data kati ya Marekani na Ulaya yalikwisha mnamo mwezi Octoba mwaka 2015,na huku mkataba mpya ukitarajiwa,bado haujaidhinishwa.