Ehud Olmert aongezewa kifungo cha jela

Ehud olmert Haki miliki ya picha AFP Getty Images
Image caption Waziri mkuu wa zamani wa Israeli Ehud Olmert akiwa mahakamani mjini Jerusalem

Mahakama ya Israeli imemuongezea kifungo cha mwezi mmoja zaidi juu ya miezi 18 ya awali waziri mkuu wa zamani Ehud Olmert kwa kupokea hongoMahakama ilikataa ombi la Bwana Olmert ambalo limngemuwezesha kutumikia kifungo cha miezi sita kwa kukiuka sheria sambamba na kifungo cha sasa cha kula mlungula.

Badala yake, atakuwa jela kwa miezi mitano wakati huo huo akitumikia kifungo hicho cha mwezi mmoja.Olmert,ambae alikua waziri mkuu kutoka 2006 hadi 2009, atakua waziri mkuu wa kwanza wa zamani katika serikali ya Israeli kwenda jela pale atakapoanza kutumikia kifungo chake Jumatatu ijayo.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Awali mahakama kuu ya Israeli ilimfutia mashtaka ya kupokea hongo ya shekel 500,000(sarafu ya Israeli)

Akiwa na umri wa miaka 70 alihukumiwa kifungo cha miaka sita mnamo mwaka 2014 baada ya kupatikana na hatia ya kukubali kitita cha dola 129 alipokua meya wa Jerusalem kama hongo kutoka kwa wajenzi wa mradi wa makazi na kupokea shekel 60,000-kama hongo iliyohusiana na mradi mwingine.

Lakini mahakama kuu ilifuta tuhuma hizo ya kupokea hongo ya shekel 500,000 na kumpunguzia hukumu hadi miezi 18.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Bwana Olmert amekana tuhuma za kulpokea malipo yoyote kinyume cha sheria

Mahakama kuu bado haijatoa uamuzi wa kesi ya rufaa ya Bwana Olmert dhidi ya hukumu ya miezi minane jela aliyopewa mwaka jana baada ya kupatikana na hatia ya ufisadi na kukiuka imani kwa kukubali malipo haramu kutoka kwa mfanyabiashara wa kimarekani.

Olmert amekanusha kupokea hongo ama kupokea malipo yoyote kinyume cha sheria , lakini alikiri kwamba alijaribu kumshawishi katibu wake wa zamani asitoe ushahidi dhidi yake.