Mji wa Aleppo unasababisha majanga

wakala wa utoaji misaada wametoa onyo kuhusiana na majanga ya kibinadamu nchini Syria ambayo yanasababishwa na mapigano yanayoendelea magharibi mwa mji wa Aleppo unasababisha majanga.

Kamati la kimataifa la shirika la msalaba mwekundu inasema usambazaji wa maji katika mji huo umesimamishwa na sasa ni wiki mbili zimepita huku kituo cha pampu kikiwa kimeharibiwa. wasambazaji wengine wa misaada wamesitisha huduma huku kukiwa na tatizo la mafuta na umeme.

Madaktari wa kujitolea wasio na mipaka wanasema hospitali zipatazo tatu zimeteketezwa na mashambulizi ya anga.

ICRC imesema misaada zaidi ya chakula, maji na madawa yanahitajika katika siku za usoni.