Tanzania yafichua wizi wa milioni 700

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Magufuli

Serikali ya Tanzania imebaini wizi wa takribani shilingi milioni 700 sawa na dola laki tatu za marekani ($320,000 )katika shirika lake la Ndege (ATCL) kupitia kampuni ya wakala wa ukatishaji tiketi ya Salama World Travel iliyopo visiwa vya Comoro.

Hii ni moja ya harakati za serikali kulifufua Shirika la Ndege Tanzania.

Kufuatia upotevu huo wa fedha, mkurugenzi wa Fedha wa ATCL Steven Kasubi amesimamishwa kazi.

Image caption Shirika la ndege la Air Tanzania

Uchunguzi umeanza chini ya kikosi cha polisi kitengo cha usalama mitandaoni ili kubaini mtandao mzima wa wote walivyohusika.