Uchunguzi wa ajali ya treni waendelea Ujerumani

bavaria_treni Haki miliki ya picha Getty
Image caption Vifusi vya treni mbili baada ya kugongana katika mji wa Bavaria

Polisi nchini Ujerumani wamepinga uvumi kwamba muongozaji wa leri alizima mifumo ya inayojiongoza ya safari za treni muda mfupi kabla ya mbili za abiria kugongana katika mji wa Bavaria.

Takriban watu 10 walikufa na wengine kadhaa kujeruhiwa, 18 vibaya.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Polisi yasisitiza mifumo ya kuongoza treni haikuzimwa wakati mkasa ilipotokea

Taarifa zisizo rasmi zimethibitisha kuwa mfumo unaojiongoza wa breki wa treni ulizimwa kuruhusu moja ya treni kuwasili kwa muda uliopangwa.

Hata hivyo msemaji wa polisi amekanusha madai hayo kama "uvumi mkubwa".

"achana na taarifa hizo, tunapinga hilo," msemaji wa polisi alimueleza mtangazaji wa Ujerumani Bayerischer Rundfunk.

Mfumo wa breki, ambao unapaswa kuingia pale treni inapofika kwenye taa nyekundu, uliwekwa baada ya mkasa wa mwaka 2011 katika eneo la Magdeburg ambapo watu 10 walifariki.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wahudumu wa shughuli za uokozi karibu na eneo la Bad Aibling ambapo ajali hiyo ilitokea

Taarifa zinazotolewa na vyombo vya habari vya Ujerumani zinasema kuwa katika hali isiyo ya kawaida mfumo huo unaojiongoza unaweza kuongozwa na wahudumu wa leri.

Kosa la kibinadamu bado linaendelea kuchunguzwa kama chanzo cha mkasa huo, uliotokea katika njia moja ya leri siku ya Jumatatu asubuhi karibu na eneo la Bad Aibling, mji uliopo kilometa 60 kusini mashariki mwa mji wa Munich.

Waziri wa uchukuzi amesema kua treni hizo mbili ziligongana wakati zilipokua zikisafiri kwa kasi ya kilometa 100 kwa saa kila moja. Wahudumu wa uokozi walifanya kazi kwa muda wa saa kadhaa, kuwaokoa majeruhi kutoka kwenye vifusi.