Ndovu aingia mjini na kuhangaisha watu India

Huwezi kusikiliza tena

Ndovu mwitu aliingia katika mji mmoja katika jimbo la Bengal Magharibi nchini India na kuhangaisha wakazi kwa saa kadha.

Maafisa walitumia vishale vyenye dawa ya kutuliza wanyama kumtuliza.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Ndovu huyo aliharibu nyumba na magari

Lakini tayari alikuwa ameharibu nyumba, magari na pikipiki kabla ya kudhibitiwa.

Hata hivyo, maafisa wa mji huo wa Siliguri wanasema hakuna mtu aliyeumizwa wakati wa kisa hicho.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Watu waliojawa na wasiwasi walikimbia kumkwepa

Ndovu huyo baadaye alipelekwa kwenye hifadhi moja ya wanyama ambayo hutumiwa kuwafuga ndovu na wanasema wanapanga kumrejesha porini baadaye.

Watu walioshuhudia wanasema ndovu huyo aliingia mjini kutoka msitu ulio karibu na alionekana kuwa na wasiwasi na kukanganyikiwa.

Kisa hicho kimetokea siku chache tu baada ya chui kuingia shuleni na kujeruhi watu sita katika eneo la Bengaluru.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Maafisa walitumia vishale vyenye dawa kumtuliza
Haki miliki ya picha AP
Image caption Walioshuhudia wanasema ndovu huyo alionekana kuwa na wasiwasi
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Maafisa walitumia kreni kumuinua na kumuingiza kwenye lori baada ya kumtuliza