Sasa unaweza kubadili akaunti ukiwa Instagram

Image caption Instagram

Mtandao wa Instagram sasa umeanza kuwaruhusu wateja wake kubadilisha akaunti tofauti.

Programu hiyo ya kusambaziana picha ilithibitisha habari hizo katika chapisho la Blogu.

  • Haya hapa maelezo ya kuingia.

Kwanza hakikisha kuwa programu imebadilika na kufikia 7.15 katika iOS na Adroid.

Wakati unapoingia,bonyeza vitone vitatu vilivyopo juu katika kona ya kulia ili kuweza kuwa na ukurasa wa chaguo ama ''option''.

Image caption ukurasa wa Instagram

Shuka chini halafu bonyeza ''Add account''.