Unyanyasaji wa kingono wajadiliwa Iran

Haki miliki ya picha Facebook Sheena Shirani
Image caption Aliyekuwa mwana habari wa kituo cha Press TV nchini Iran Sheena Shirani.

Madai ya unyanyasaji wa kingono nchini Iran katika kituo kimoja cha runinga yamesababisha wanawake nchini Iran kuvunja ukimya wao na kuanza kulijadili swala hilo kwa kina ambalo kwa utamaduni wao ni mwiko.

Sheena Shirani,msomaji habari katika runinga ya Press TV ambayo hutumia lugha ya kiingereza ,alivunja mwiko huo kwa kuzungumza unyanyasaji wa kingono aliokumbana nao mbele ya wasimamizi 2 wa kituo hicho kwa kipindi kirefu.

Haki miliki ya picha Facebook Sheena Shirani
Image caption Majibizano ya maandishi kati ya Shirani na Emadi

Madai yake yalisambazwa hadharani wakati alipochapisha mtandaoni mazungumzo ya simu ambayo mtu anayedaiwa kuwa msimamizi wake kazini Hamid Reza Emadi mara kadhaa alitaka kulala naye.

Haki miliki ya picha
Image caption Sheena Shirani akisoma habari

Kufuatia kisa hicho Shirani aliwacha kazi na kuondoka katika taifa hilo na baadaye kuchapisha rekodi hiyo ya sauti ambayo imesikizwa zaidi ya mara 120,000 katika ukurasa wake wa mtandao wa facebook na mtandao mmoja wa habari uliopo nje ya taifa hilo.

Vilevile alichapisha majibizano yake ya maandishi na Emadi ambapo anamtaka kuondoa sauti hiyo katika mtandao wake.