Korea Kaskazini kukatiza mawasiliano na Kusini

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Korea Kaskazini sasa imeonya kuwa itakata mawasiliano na Korea Kusini

Korea Kaskazini sasa imeonya kuwa itakata mawasiliano na Korea Kusini kufuatia hatua ya Korea Kusini kusimamisha shughuli za pamoja katika viwanda vya pamoja vya Kaesong.

Korea Kusini ilichukua hatua hiyo baada ya Pyongyang kutupa roketi iliyokuwa imebeba satelaiti katika anga ya mbali.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kampuni za Korea Kusini zimeanza kuwaondoa wafanyakazi wake na mali katika uwanja wa viwanda vya pamoja ulioko Korea Kaskazini

Vilevile Seoul imekasirishwa na majaribio ya hivi punde ya kinyuklia yaliyotekelezwa na Pyongyang .

Pyongyang inasema kuwa hatua ya Seoul ya kufunga shughuli za viwanda vya pamoja vya Kaesong ni dhihirisho la vita.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Seoul imekasirishwa na majaribio ya hivi punde ya kinyuklia yaliyotekelezwa na Pyongyang

Seoul hata hivyo inasema imechukua hatua hiyo ilikuinyima Pyongyang kitega uchumi chake kwani imekuwa ikitumia faida zote inazopata kunoa makali yake ya kivita na kuendeleza mradi wake wa kinyuklia.

Kampuni za Korea Kusini zimeanza kuwaondoa wafanyakazi wake na mali katika uwanja wa viwanda vya pamoja ulioko Korea Kaskazini ambao unatumiwa na mataifa yote mawili.

Siku ya Jumatano, Serikali ya Seoul ilitangaza kuwa itasitisha shughuli zake zote katika eneo la viwanda la Kaeosong - ishara ya pekee iliyoko juu ya ushirika kati ya mataifa hayo mawili.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Askari wa Korea Kaskazini wakishika doria kwenye mpaka wake na Korea Kusini

''Korea Kusini ina kila sababu ya kulipiza kisasi dhidi ya Korea Kaskazini kwa kufanya jaribio la kufyatua hewani makombora ya masafa marefu'' taarifa hiyo ilisema.

Mameneja kadhaa wa Korea Kusini waliambia BBC kuwa walishtuka kasi ambayo imetumika kusitisha shughuli za biashara zao.

Biashara katika eneo hilo la biashara linajulikana kuletea Korea Kaskazini pesa nyingi za kigeni, ambazo Korea Kusini innasema zimetumiwa kuimarisha zana za kinyukilia za Korea Kaskazini.