Mahakama:Bi Netanyahu aliwadhulumu wafanyikazi

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Sara Netanyahu

Mkewe waziri mkuu nchini Israel Benjamin Netanyahu ,Sara aliwatusi na kuwatendea maovu wafanyikazi wake wa nyumbani ,mahakama moja ya wafanyikazi imebaini katika kesi iliowasilishwa na aliyekuwa msimamizi wa nyumba hiyo.

Mahakama hiyo ilikubali madai ya Meni Naftali kwamba alitusiwa vibaya na baadaye kumlipa dola 43,000 kama fidia.

Uamuzi huo umesema kuwa hasira za Bi. Netanyahu ziliathiri mazingira ya wafanyikazi wake.

Bi. Netanyahu alisema kuwa madai hayo yalikuwa ya uongo akisema kuwa ana uhusiano mzuri na wafanyikazi.

Afisi ya waziri mkuu haikutoa tamko lolote kuhusu uamuzi huo.Ilikana madai ya hapo mbeleni dhidi ya Bi Netanyahu kama maovu na ya kusengenya.

Kesi ya awali ambapo alituhumiwa kwa kumtusi muuzaji duka mmoja ilitatuliwa nje ya mahakama.