Syria: Urusi yapendekeza kusitisha vita

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Marekani pia inaamini kuwa Urusi imejipatia majuma matatu kuwapondaponda waasi kabla ya kusitisha kampeini yake ya angani.

Azimio la Marekani na washirika wake kutaka mapigano yanayoendelea nchini Syria kusitishwa mara moja kabla mazungumzo ya upatanishi kufanyika yamegonga mwamba.

Urusi ambayo ni mwanachama wa kudumu wa baraza la mawaziri imeipinga kwa kinywa kipana na ikatishia kutumia uwezo wake kutupilia mbali hoja yeyote ya Marekani.

Urusi yenyewe ambayo ni Mshirika mkubwa wa rais wa Syria Basher al Assad imependekeza Machi mosi.

Lakini wakosoaji wake ikiwemo Marekani wanasema kuwa nchi hiyo ambayo inaendelea kuishambuilia maeneo yanayothibitiwa na waasi kwa ushirikiano na jeshi la Syria wanawalenga waasi wanaoungwa mkono na Marekani badala ya kuwalenga wapiganaji wa kundi la waislamu la Islamic State.

Marekani pia inaamini kuwa Urusi imejipatia majuma matatu kuwapondaponda waasi kabla ya kusitisha kampeini yake ya angani.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Majeshi ya Serikali yameingia Aleppo

Naibu waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Urusi, Gennady Gatilov, amesema kuwa uwezekano huo utajadiliwa huko Munich Ujerumani , mahala ambapo kongamano la kimataifa linafanyika baadaye leo ili kutafuta namna ya kukomesha vita nchini Syria.

Wawakilishi wa vyama vya upinzani nchini Syria, Uturuki, na Marekani wameshutumu mashambulizi ya angani yanayotekelezwa na majeshi ya Urusi yanayounga mkono majeshi ya serikali ya nchi hiyo na kukiuka muafaka wa amani wa kukomersha mashambulio uliotiwa saini huko Geneva mwei Januari.

Zaidi ya watu wapatao 500 wanasemekana kuuawa katika mashambulio ya hivi punde yaliyotekelezwa na ndege za kijeshi za Urusi karibu na mji wa Aleppo.

Mamia kwa maelfu ya wengine wamekimbilia usalama wao.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wakati huohuo kumekuwa na ripoti kuwa ndege za urusi zimewasaidia wapiganaji wakikurdi kuwang'oa waasi kutoka kwenye kambi ya wanahewa ya zamani waliokuwa wameiteka kaskazini mwa Aleppo.

Mashirika ya kutoa misaada imeonya kuwa kampeini kali inayoendeshwa na Majeshi ya Syria kwa ushirikiano na jeshi la wanahewa wa Urusi dhidi ya ngome ya waasi ya Aleppo imepelekea kuhamishwa kwa zaidi ya watu 50,000.

Shirika la msalama mwekundu pia umeomba uruhusiwe kuingiza msaada kwa ngome hiyo ya waasi wanaompinga rais Basher al Assad.

Wakati huohuo kumekuwa na ripoti kuwa ndege za urusi zimewasaidia wapiganaji wakikurdi kuwang'oa waasi kutoka kwenye kambi ya wanahewa ya zamani waliokuwa wameiteka kaskazini mwa Aleppo.