Twitter yafanyia mabadiliko ukurasa wake

Image caption Tweeter mpya

Mtandao wa Twitter unafanya mabadiliko kuhusu vile ukurasa wa wateja wake utakavyoonekana.

Programu hiyo itaonyesha tweets kadhaa zilizopewa kipaumbele,kwa kuzingatia kile ambacho wateja wanafikiria ni muhimu,mbele ya orodha ya kawaida inayobadili mpangilio.

Na kipengele kipya kitawaruhusu maafisa wa mauzo kuweka kanda ya video .

Tangazo hilo linajiri wakati wa kutangazwa kwa matokeo ya kifedha ya mtandao huo.

Vipengele hivyo vimetengezwa hali ya kuwa vitawasaidia watumiaji kushiriki na vilevile kuwavutia wawekezaji.

Image caption Ukurasa wa Tweeter

Hatahivyo mtaalam mmoja amesema kuwa umuhimu mkubwa unaopewa kanda za video huenda ukakwama.

''Sababu ambayo imesababisha mafanikio makubwa ya facebook ni kwamba imeweza kuweka machapisho na video zilizofadhiliwa katika mkusanyiko wa ujumbe,''alisema Richard Holway, mwenyekiti wa kampuni ya TechmarketView.

Lakini Tweeter iko tofauti kwa kuwa watu hutumia mda mchache kuangalia kila chapisho na kuweka video juu ya ujumbe wao huenda kukawaudhi wengi.