Gazeti la Independent kuacha kupigwa chapa

Haki miliki ya picha

Wamiliki wa magazeti ya Independent na Independent on Sunday wametangaza kwamba magazeti hayo ya Uingereza hayatapigwa chapa tena kuanzia mwezi Machi.

Kampuni ya ESI Media imesema magazeti hayo yatahamia katika mfumo wa dijitali.

Kampuni hiyo imesema “kuna wafanyakazi kadha wa idara ya uhariri ambao watapoteza kazi”.

Hata hivyo kuna kutakuwa na nafasi 25 mpya za kazi za kuangazia mfumo dijitali.

ESI pia wamethibitisha kwamba kampuni tanzu ya i Newspaper itauzwa Johnston Press, hili likisubiri idhini kutoka kwa wenyehisa wa Johnston.

Nakala ya mwisho ya gazeti la Independent itachapishwa Jumamosi tarehe 26 Machi nayo ya mwisho ya Independent on Sunday ichapishwe 20 Machi.

Magazeti mengi duniani yamekuwa yakitatizika kutokana na kushuka kwa idadi ya wanunuzi wa magazeti kutokana na teknolojia.

Idadi ya watu wanaotegemea mitandao kujipasha habari inaendelea kuongezeka.