India yazindua bunduki nyepesi duniani

Image caption Bunduki nyepesi zaidi duniani

Miaka miwili baada ya India kuzindua Nirbheek,bunduki inayodaiwa kuwa ya kwanza ya wanawake,kiwanda cha kutengeza silaha cha taifa hilo kimezindua bunduki kama hiyo na kusema ndio bunduki nyepesi zaidi duniani.

Bunduki hiyo ina gramu 250 na inauzwa dola 513.Nirbheek iliuzwa kwa bei ya juu ya dola 1,990.

Watengezaji wake wanasema kuwa Nidar imeundwa kwa kutumia alumini ambayo inaifanya kuwa nyepesi zaidi lakini bado ina nguvu sawa na ile ya chuma.

Urefu wake ni wa milimita 140 ambao unaifanya kuweza kutosha katika kiganja cha mkono.

Image caption Bunduki iliotengenezwa nchini India ili kutumiwa na wanawake kufuatia visa vingi vya ubakaji.

Bunduki zote mbili,Nirbheek na Nidar zina maana ya Nirbhiya,jina la utani alilopewa Jyoti Sign na vyombo vya habari,ikiwa ni mwathiriwa wa genge la ubakaji katika basi moja mjini Delhi mwaka 2012.

Majina yote matatu yanamaanisha jasiri kwa lugha ya Hindi.

Hutengezwa na viwanda vya serikali na watengezaji wake wanasema kuwa zitawasaidia watu kutokuwa na uwoga na jasiri.