Nigeria yawaachilia washukiwa wa B. Haram

Haki miliki ya picha Screen Grab
Image caption Wapiganaji wa Boko Haram

Jeshi la Nigeria limewaachilia watu 275 lililowakamata kwa tuhuma za kuwa wanachama wa kundi la wapiganaji wa Boko Haram,afisa mmoja amesema.

Washukiwa hao waliachiliwa baada ya uchunguzi kubaini kwamba walikuwa hawana uhusiano na wapiganaji hao na kukabidhiwa kwa Gavana wa jimbo la kaskazini la Borno.

Walikuwa watu 142,ikiwemo wanawake 49,vijana 22 na wasichana 50.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wanajeshi wa Nigeria

Raia wawili wa Nigeria na wawili wa Cameroon,msemaji wa Gavana Usman kumo aliiambia BBC Hausa.

Hatua hiyo inajiri kufuatia tuhuma zilizotolewa na shirika la Amnesty International kwamba wanajeshi hao waliwaua wafungwa 8,000 kama mojawapo ya hatua zake za kukabiliana na kundi la Boko Haram.

Mapema mwezi huu,kundi hilo la haki za kibinaadamu lilikosoa serikali ya Nigeria kwa kumrudisha kazini jenerali mmoja wa jeshi ambaye linamtuhumu kwa uhalifu wa kivita.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Boko Haram

Jeshi limesema kuwa madai hayo yanachunguzwa.