Polisi waondoa vinyago vya wagombea Uganda

Vinyago
Image caption Vinyago vya wagombea vimewekwa maeneo mengi mijini

Polisi wameanza kuondoa vinyago vyote vya wagombea wa urais nchini humo ambavyo vimewekwa katika barabara za miji, gazeti la Daily Monitor linaripoti.

Gazeti hilo linasema vinyago vilipigwa marufuku 2010 kwa msingi kwamba vinaweza kutumiwa na wanamgambo kutekeleza mashambulio.

Uchaguzi mkuu nchini Uganda utafanyika tarehe 18 Februari.

Julai mwaka 2010, watu 74 waliuawa na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa kwenye mashambulio mawili mjini Kampala.

Kundi la al-Shabab kutoka Somalia lilidai kuhusika likisema ilikuwa hatua ya kulipiza kisasi kushiriki kwa majeshi ya Uganda katika kikosi cha Umoja wa Afrika ambacho hadi sasa kinakabiliana na al-Shabab nchini Somalia.