Bashar al-Asaad aapa kuikomboa Syria

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Bashir al-Asaad

Rais wa Syria Bashar al Asaad ameapa kulikomboa taifa lote la Syria katika mahojiano na kituo cha habari cha AFP saa chache tu baada ya makubaliano ya kusitisha vita.

Ameiambia AFP kwamba kushiriki kwa mataifa mengine nchini Syria kunamaanisha suluhu itachakua muda mrefu.

Awali ,Umoja wa mataifa ulisema kuwa unatumai kuanza kupeleka chakula katika maeneo yaliozungukwa katika kipindi cha saa 24.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Syria

Hatua hiyo inajiri baada ya mataifa yenye uwezo mkubwa duniani kukubaliana kusitisha mapigano katika kipindi cha juma moja.

Zaidi ya watu 250,000 wameuawa na zaidi ya milioni 11 kuwachwa bila makao katika mapigano ya miaka mitano nchini humo.

Baadhi ya miji kadhaa ya Syria imekatwa na haiwezi kupokea misaada kwa kiindi cha mwaka mmoja kutokana na vita.

Takriban watu milioni 13.5 wanahitaji msaada ,UN imesema.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Asaad na Putin

Akizungumza mjini Damscus ,bwana Assad amesema kuwa wanajeshi wa serikali watajaribu kuikomboa Syria bila kusita,lakini kushiriki kwa mataifa mengine kunamaanisha kuwa suluhu itakuwa na gharama kubwa.