Cameron:''Tuko EU kwa masharti''

Haki miliki ya picha AFP
Image caption David Cameron

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron amesema kuwa atapendelea nchi yake iendelee kuwa mwanachama wa muungano wa Ulaya ikiwa Ulaya itakubaliana na mabadiliko yaliyopendekezwa na Uingereza.

Akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha jioni mjini Hamburg nchini Ujerumani iliyohudhuriwa na Chansela wa Ujerumani Angela Merkel bwana Cameron alisema kwa lilikuwa ni jukumu la Ulaya kuwa Uingereza iendelee kusalia kwenye muungano huo.

Lakini ameonya kuwa ikiwa hakutakuwa na makubaliano kuhusu masuala ya uanachama basi hawezi kufanya uamuzi wowote.

Ilikuwa hotuba ya mwisho ya bwana Cameron kabla ya mkutano wa muungano wa Ulaya wa wiki ijayo ambapo anatarajia kuwa mapendekezo yake yataidhinishwa.