Wanaowatamani watoto kingono watumia facebook

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Watu wanaowatamani watoto kingono watumia mitandao

Watu wanaowatamani kingono watoto wadogo wanatumia makundi ya siri katika mtandao wa facebook kuchapisha na kubadilishana picha chafu za watoto ,BBC imebaini.

Hali ya ulivyopangwa mtandao huo wa kijamii unayaficha makundi hayo kwa wateja wengi na ni wanachama pekee ambao wanaweza kuona yanayoendelea.

Kamishna wa watoto nchini Uingereza Anne Longfield amesema kuwa facebook haifanyi juhudi za kutosha kuyazuia makundi hayo ili kuwalinda watoto.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption facebook

Hatahivyo afisa anayesimamia sera za umma katika mtandao huo ameiambia BBC kwamba yuko tayari kuondoa yaliyomo na ambayo hayafai kuwemo.

Uchunguzi wa BBC umebaini idadi ya makundi kadhaa ya siri ,yaliobuniwa na kuendeshwa na wanaume wanaowatamani kingono watoto wadogo likiwemo moja ambalo linaendeshwa na mwanamume mmoja aliyefungwa kwa kuwatamani watoto wadogo na ambaye hadi sasa yupo katika orodha ya wahalifu wa ngono.

Makundi hayo yana majina yanayoonyesha wazi yaliomo ndani yake na yanamiliki picha za uchi na zile za ngono nyingi zikiwa za watoto.

Pia yana maoni ya ngono yanayochapishwa na wateja wake.

Haki miliki ya picha NCA
Image caption Genge la watu wanaowatamani watoto nchini Uingereza ambao waliwabaka watoto.

Katika makundi mengine ya siri tulibaini picha za watoto wamejiweka katika hali ya kuwavutia watazamaji wao.

Pia kuna picha ambazo zimeibwa kutoka kwa mtandao wa facebook na magazeti ambazo zinaandamana na maoni machafu.

Kwa mfano Diana {sio jina lake} aligundua picha za mwanawe wa kike zimeibwa katika blogu yake.

Zilichapishwa katika mtandao unaotumiwa na watu wanaowatamani watoto kingono na zimekuwa zikisambazwa miongoni mwa wanachama wake ambao pia walichapisha maoni machafu kuzihusu.