Ndege za Saudia kushambulia kutoka Uturuki

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ndege za kijeshi

Waziri wa mashauri wa nchi za nje wa Uturuki, Mevlut Cavusoglu, anasema kuwa Saudi Arabia itaweka ndege za kijeshi katika kituo cha jeshi cha Uturuki, ambako zitashambulia wapiganaji wa Islamic State nchini Syria.

Bwana Cavusoglu, (shawushoglu), piya alisema inawezekana kwa wanajeshi wa nchi yake na Saudi Arabia, kushiriki kwenye mapigano ya ardhini dhidi ya IS.

Waturuki na wa Saudia wanaunga mkono wapiganaji nchini Syria, ambao hivi karibuni wamerudi nyuma, kwa sababu ya mashambulio ya jeshi la Syria, likisaidiwa na Urusi.

Urusi imeonya nchi nyengine zisiingilie kati ya vita vya ardhini nchini Syria, na imesema tukio hilo linaweza hata kuzusha vita vya dunia.