Watoto 462 wapatikana na Zika Brazil

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mwanamke mjamzito nchini Brazil

Mamlaka ya afya nchini Brazil imeripoti kuongezeka kwa visa vilivyothibitishwa vya matatizo ya ubongo kwa watoto wanaozaliwa kutokana na virusi vya Zika.

Wizara ya afya imesema kuwa watoto 462 kwa sasa wamethibitishwa kuwa na matatizo ya ubongo.

Wanachunguza karibu visa vingine 4000 vilivyoripotiwa.

Haki miliki ya picha Flavio Former
Image caption Mama mwenye mtoto aliye na ugonjwa wa Zika

Virusi hivyo vinavyosambazwa na mbu vimesambaa kwa haraka kati ya mataifa ya Marekani kwa zaidi ya mwaka mmoja uliopita.

Zaidi ya wanajeshi 200,000 watapelekwa hii leo kote nchini Brazil kuwaonya watu kuhusu hatari za virusi vya Zika.