wapalestina wawapiga risasi wa Israel

Haki miliki ya picha Reuters

Wapalestina watano wamepigwa risasi na vikosi vya usalama vya ki Israel kwa madai ya kufanya majaribio kadhaa ya kutaka kuwashambulia.msemaji wa walinda usalama hao alieleza kwamba wapalestina wawili waliuawa baada ya kuwashambulia kwa risasi mjini Jerusalem.

Mapema mjini humo, polisi waliwapiga risasi vijana na kufa waliodai kwamba walikuwa wakifanya jaribio la kutaka kuwachoma kwa vitu vyenye ncha kali. Vifo vingine vilitokea katika mji wa Jenin upande wa West Bank, mahali ambako jeshi la Israel wandai kuwaua watoto wenye umri wa miaka kumina mitano waliouwa kwenye kundi la vijana.

Mjini Hebron, binti mwenye asili ya ki Palestina mwenye umri wa miaka kumi na saba alipigwa risasi na kujeruhiwa vibaya akidaiwa kutaka kufanya jaribio la kutaka kumshambulia afisa wa polisi.