Baba Mtakatifu awaasa wa Mexico

Image caption Papa Francis akivishwa kofia ya kitamaduni nchini Mexico

Baba mtakatifu Francis amewataka wananchi wa Mexico kuifanya nchi yao kuwa nchi ya fursa,mahali ambako haitakuwa lazima kuhama na pia vijana hawataangukia katika mikono ya kile alichokiita biashara ya kifo.

Matamshi hayo ya baba mtakatifu aliayatoa katika ibada ya wazi iliyohudhuriwa na watu wanaokadiriwa kufikia laki tatu katika eneo lenye makazi duni ya watu nchini Mexico.

Watu zaidi ya milioni moja unusu wanaishi katika eneo la Ecatepec, linalotawaliwa na biasshara haramu ya dawa za kulevya na vurugu za kila namna ikiwemo uhalifu dhidi ya wanawake.

Baba matakatifu ameanza ziara ya siku tano nchini humo tangu mwishoni mwa wiki, nchi ambayo ni ya pili kwa kuwa na waumini wengi wa dhehebu la kikatoliki ulimwenguni ikitanguliwa na Brazil.