Papa: Watendee haki wahanga wa mihadarati Mexico

Image caption Papa Francis

Kiongozi mkuu wa kanisa katoliki duniani Papa Francis ameadhimisha misa katika kanisa la Virgin of Guadalupe nchini Mexico City.

Hiyo ni ziara yake ya kwanza ya siku nzima nchini humo.

Image caption Papa Francis ameadhimisha misa katika kanisa la Virgin of Guadalupe

Awali, aliwaomba viongozi wa kisiasa na kidini wa Mexico kufanya kila wawezalo ili kuhakikisha kuna usalama wa kutosha na haki ya kweli kwa raia wa taifa hilo.

Papa Francis anasema kuwa ulanguzi wa dawa za kulevya na ghasia zinazoambatana nayo ni saratani mbaya mno inayoharibu jamii ya wa Mexican.

Image caption Papa Francis anasema kuwa ulanguzi wa dawa za kulevya--- na ghasia zinazoambatana nayo -- ni saratani mbaya

Mwaandishi habari wa BBC nchini Mexico, anasema kuwa tayari ameibua maswala tata ambayo serikali haipaswi kupuuza.