UN: Watu 3,500 waliuawa Afghanistan mwaka jana

Image caption UN: Watu 3,500 waliuawa Afghanistan mwaka jana

Umoja wa Mataifa unasema kuwa idadi ya watu waliouwawa nchini Afghanistan imeongezeka kwa asili mia 4% mwaka uliopita, na kufikia kiwango kikubwa kabisa.

Watu elfu-tatu na nusu 3,500 waliuwawa na elfu saba-na-nusu (7,500) walijeruhiwa.

Ingawa idadi ya raia waliokufa ilipungua, waliojeruhiwa waliongezeka.

Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa wapiganaji walisababisha hasara kubwa zaidi.

Kati ya watu wanne waliuawa 1 alikuwa ni mtoto.

Takwimu zinaonesha kuwa asilimia 37% ya wahasiriwa walikuwa wanawake huku watoto wakiwa ni 14% .

Serikali ya Afghanistan imewalaumu wapiganaji wa Taleban kwa kulenga wanawake na watoto katika mashambulizi yake kwa nia ya kuzua hofu miongoni mwa umma.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kati ya watu wanne waliuawa 1 alikuwa ni mtoto.

Afisa mkuu wa umoja wa mataifa anayeshughulikia maswala ya haki za kibinadamu anasema kuwa mashambulizi dhidi ya ''wanawake na watoto'' ama kwa jumla watu wasio na silaha ni makosa ya kivita.

Zeid Ra'ad al-Hussein ameiambia BBC kuwa mashambulizi mengi nchini humo yamechukua mkondo huo wa kukusudia kuwadhuru watu wasiokuwa na silaha.

Tangu kuondoka kwa majeshi ya muungano NATO nchini Afghanistan yapata miaka 5 iliyopita idadi ya watu waliouawa kutokana na mashambulizi ya Taleban yameongezeka mno.

Asilimia kubwa ya vifo hivyo vinatokana na walipuaji wa kujitolea mhanga wanaolenga maeneo yenye watu wengi mashambulizi ya kuvizia na mashambulizi ya kuteka nyara yanayotekeleza dhidi ya umma.