Jaji wa mahakama ya juu Marekani afariki

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jaji wa mahakama ya juu Marekani Antonon Scalia afariki

Jaji mmoja maarufu ambaye amehudumu kwa muda mrefu katika mahakama kuu nchini Marekani, Antonin Scalia, ameafariki dunia .

Scalia amefariki akiwa na umri wa miaka 79.

Kifo chake kinasemekana kuwa cha kawaida tu.

Amehudumu kama jaji kwa miaka thelathini na alitazamwa na wengi kama sauti imara ndani ya wanachama wenye msimamo mkali.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Scalia ( wa pili kutoka kulia aliyeketi) amefariki akiwa na umri wa miaka 79.

Chama cha Conservatives sasa kimepoteza nafasi yake muhimu ndani ya mahakama hiyo kuu iliyo na majaji tisa.

Rais Barrack Obama anasema kuwa ana nia ya kutekeleza agizo lake la kisheria, kwa kumteua mtu kujaza nafasi hiyo.

Lakini anatarajiwa kukabiliwa vikali na bunge la Senate, ambalo lina wanachama wengi wa chama cha Republican, ambayo ni sharti iidhinishe chaguo hilo lake.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wagombea wa chama cha Republican

Wakati huo huo wagombeaji sita waliosalia katika kinyang'anyiro cha kutafuta nafasi ya kuwania kiti cha urais katika chama cha Republican nchini Marekani, wamesema kuwa hatua ya kumchagua jaji mpya wa mahakama kuu nchini humo, inafaa kusubiri hadi pale uchaguzi mkuu umalizike mwezi Novemba.

Swala hilo limeibuka katika mjadala wa hivi punde zaidi wa majadiliano ya moja kwa moja ya runinga kwa wagombezi wa chama cha Republican.

Baadhi ya wagombea kiti hicho wamekubaliana kwamba Rais Obama bila shaka atajaribu kumteuwa jaji mwenye msimamo wa kadri ili kuchukua mahala pa jaji Scalia, lakini anatarajiwa kukabiliwa vikali.

Mjadala wa moja kwa moja wa runinga unanyika juma moja kabla ya kufanyika kwa kura ya mashinani katika jimbo la South Carolina.