EU kuijadili Uingereza

Image caption Rais wa baraza la umoja wa Ulaya, Donald Tusk

Rais wa baraza la umoja wa ulaya , Donald Tusk, ametoa angalizo kwamba kuna hatari iliyo dhahiri kwamba umoja wa Ulaya huenda ukasambaratika endapo Uingereza itaamua kujiondoa katika umoja huo.

Donald Tusk ametoa kauli hiyo akiwa nchini Romania, na kusema kwamba mazungumzo na nchi ya Uingereza yako katika wakati muhimu na yanapaswa kuchukuliwa kwa uangalifu mkubwa.

Haki miliki ya picha PA

Naye waziri mkuu wa Uingereza David Cameron amekuwa akishinikiza kuwe na makubaliano kabla ya kura ya maoni vinginevyo nchi hiyo ijiondoe katika jumuia ya umoja wa ulaya.

Nchi ya Uingereza inataka mabadiliko ikiwemo kukabiliana na faida ya ustawi unaotolewa kwa wahamiaji.Bwana Cameron ana matarajio ya kufikiwa mwafaka katika mkutano wa jumuiya ya Ulaya utakaofanyika mjini Brussels wiki hii.