Kupambana dhidi ya maradhi ya akili

Haki miliki ya picha Thembela Nymless Ngayi
Image caption Thembela Nymless Ngayi mpiga picha

Thembela Nymless Ngayi ni mpiga picha mwenye umri wa miaka, 29 na mzaliwa wa mji wa Umtata iliyoko Mashariki mwa Afrika Kusini.

Hivi sasa sasa anaishi mjini Cape Town.

Kupitia mfululizo wake wa picha, yenye kichwa ''The Great African Horror Story : Depression'', yeye hukabiliana na unyanyapaa unaokumba watu wanaougua maradhi ya akili - hasa kwa watu weusi - katika jamii yao.

"Afya ya akili ni suala ambalo daima nimekuwa na ufahamu nao.

''hata hivyo jamii haijawahi kweli kuona au kusikia watu wakilishughulikia hadharani''.

Kwa kipindi kirefu nimeona watu karibu nami walioathirika na afya ya akili [masuala], huzuni hasa ama msongo wa mawazo, na wakati huo sikujua zaidi kuhusu hali hiyo manake niliipuzilia mbali nikisema kuwa huo ni ugonjwa unaowaathiri wazungu.

Haki miliki ya picha Thembela Nymless Ngayi
Image caption Kwa kawaida watu hupuuza suala hili na hata tunalaumu wazee wetu

"Maoni yangu hata hivyo yalibadilika mwaka jana nilipokumbwa na msongo wa mawazo na nikajipata nahuzunika sana katika kwa hakika ulikuwa wakati mgumu sana maishani mwangu.

Niligundua kwamba si mengi ya watu wanaofahamu jinsi ya kukabiliana na mtu anayesumbuliwa na maradhi ya mental akili.

Kwa kawaida watu hupuuza suala hili na hata tunalaumu wazee wetu waliotutangulia mbele za haki kama mazingaombwe, uchawi ama hata mizimwi.

''Mtu anahisi kama yeye hathamani tena''

''Anahisi hana faida tena na wala hakuna anayeona wala kuhisi maumivu yake".

"Unyogovu huathiri wanaume na wanawake, kwa hivyo imenifanya kuchagua jinsia hizo mbili kama walengwa wangu''.

Mwanamke ana majukumu mawili katika mfululizo huu.

Katika makala ya kwanza anawakilisha jamii, ya watu weusi nilikolelewa miongoni mwa.

Haki miliki ya picha Thembela Nymless Ngayi
Image caption Mwanamke ana majukumu mawili katika mfululizo huu

Katika baadhi ya picha utaona akiwapuuza wanaume wakati yeye mwenyewe anawavutia wao hao wanaume vilevile mtu anavyohisi jamii ikimtenga wakati ambao amekumbwa na maradhi haya ya akili.

Hata marafiki wako wa karibu watakutenga''

Na pale atakapohisi amepoteza kila kitu, utamuona akitafuta ufumbuzi wa yanayomkumba kwa ulevi.

"Wakati umekumbwa na msongo wa mawazo kila kitu kinakosa mantiki.

Kuna upungufu wa raha, ladha na furaha .

Kila siku ni sawa na ile iliyotangulia hakuna lipya . "

"Tunaona mwanamke akimhurumia mwanaume aliyepigwa picha katika msururu huu kufuatia kifo chake.

Vivyo hivyo ndivyo jamii inavyofanya pale mtu anapojitia kitanzi kwa kukosa ufumbuzi wa masaibu yanayomkumba.

"Kila mtu ana historia ya maisha yake na kila mmoja wetu anatumia mbinu tofauti ya kusimulia yaliyomsibu maishani.

Haki miliki ya picha Thembela Nymless Ngayi
Image caption Hata marafiki wako wa karibu watakutenga

Unaweza kutumia mfumo wa wimbo au filamu kuelezea masaibu yaliyokupata na iwapo suala hilo lina mshiko miongoni mwa jamii bila shaka itachangia mabadiliko ya mtazamo na hata kushawishi jamii kulishughulikia chanzo cha masaibu yao.

Natumaini mfululizo huu umewahamasisha watu kufungua macho yao na kulizungumzia haswa swala hilo la maradhi ya akili miongoni mwa jamii.