Pacquiao azua hamaki kuhusu wapenzi wa jinsia moja

Image caption Manny Pacquiao

Bondia Mfilipino Manny Pacquiao amezua hamaki baada ya kuwataja wapenzi wa jinsia moja kuwa ''watu wabaya hata zaidi ya wanyama''

Katika mahojiano ya moja kwa moja kwenye runinga ya kitaifa bondia huyo ambaye pia ni mwanasiasa alizua mjadala mkali na majibizano kati ya wanaharakati wa kupigania haki za wapenzi wa jinsia moja na umma.

Bondia huyo bingwa wa zamani wa uzani wastani duniani ni mkristo imara ambaye anawania kiti cha useneta katika uchaguzi mkuu ujao unaoratibiwa kufanyika mwezi Mei.

Ufulipino una asilimia kubwa ya wakatoliki ambao wanapinga kimya kimya mapenzi ya jinsia moja.

Mbunge huyo ( Pacquiao), alikuwa akihojiwa katika runinga ya TV5 mapema hapo jana.

Video inayoonesha wakati alipotamka maneno hayo katika lugha ya Tagalog, inamuonesha bondia huyo akisema

Haki miliki ya picha AP
Image caption Pacquiao amezua hamaki baada ya kuwataja wapenzi wa jinsia moja kuwa ''watu wabaya hata zaidi ya wanyama''

"Ni ukweli usiopingika kuwa wanyama ambao tunawafuga wanaheshimu maadili kuna ya kiume na ile ya kike'' .

''Je ushawahi kuona mnyama wa kiume akimkurubia mwenzake wa kiume ?''

''Au hata mnyama wa kike akimpandilia yule wa kike ?''

''Haiwezekani ?

''Kwa hivyo wanadamu wamegeuka na kuwa wabaya hata kuwazidi wanyama''!

Image caption Pacquiao aliwajibu wapinzani wake kwa kuchapisha picha yake na mkewe katika mtandao wa Instagram

Mchekeshaji mFilipino Vice Ganda na msanii Aiza Seguerra, ambao wote ni wapenzi wa jinsia moja wametuhumu Pacquiao kwa kuchochea uhsama dhidi yao.

Vilevile wamemtaja kuwa nabii wa uongo na msaliti.

Vile vile vuguvugu la kupigania haki zao ''Ladlad'' limekashifu bondia huyo na kuwataka wafuasi wao wasimpigie kura.

Mr Pacquiao, ambaye alitawala vitengo 8 tafauti za ndondi duniani alijibu matamshi yao kwa kuchapisha picha yake na mkewe katika mtandao wa Instagram.