UN yataka wahitaji wapate misaada

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Staffan de Mistura

Umoja wa mataifa umesema kwamba serikali ya Syria inao wajibu wa kuruhusu misaada ya kibinaadamu kufika katika maeneo yaliyozingirwa na mapigano.

Syria ilikwisha ruhusu ugawanywaji wa misaada katika maeneo saba nchini mwake lakini kiongozi wa kikosi maalumu cha usambazaji misaada ya kibinaadamu kutoka umoja wa mataifa , Staffan de Mistura, amesema kwamba umoja wa mataifa unahitaji kuwafikia wa Syria wote wenye uhitaji.

Misaada ya kibinaadamu ilikuwa ni mojawapo ya makubaliano ambayo Syria iliingia katika makubaliano yaliyofikiwa mjini Munich wiki iliyopita.

Wakati huo huo kuna taarifa kutoka nchini Uturuki zinazoeleza kwamba rais Recep Tayyip Erdogan na mfalme wa Saudi Arabia Salman wamezungumza kwa njia ya simu na kukubaliana kusitisha mashambulio dhidi ya raia nchini Syria.