Urusi yapinga madai ya uhalifu wa kivita

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Hospitali ya Maarat_al_nuuman nchini Syria

Urusi imepinga madai ya uhalifu wa kivita dhidi yake kufuatia shambulio la hospitali moja nchini Syria.

Msemaji wa serikali Dmitry Peskov amesema kuwa wale wanaotoa taarifa kama hizo hawana ushahidi wa kuthibitisha.

Hadi watu 50 waliuawa katika shambulio lililolenga hospitali nne na shule moja katika eneo linalodhibitiwa na waasi kaskazini mwa Syria siku ya jumatatu.

Umoja wa mataifa umesema kuwa kuzilenga hospitali na shule ni uhalifu wa kivita.

Urusi imeshtumiwa na Uturuki kwa kuhusika na mashambulio hayo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Hospitali inayodaiwa kushambuliwa na Urusi

Mashambulizi hayo ya jumatatu yalilenga hospitali mbili ikiwemo moja ya wanawake na watoto pamoja na shule inayowahifadhi watu walioachwa bila makao katika eneo la Azaz,karibu na mpaka na Uturuki,Kulinagana na umoja wa mataifa.

Watu 34 waliuawa na makumi kujeruhiwa.

Hospitali mbili pia zilishambuliwa katika eneo la Maarat al_Numan,kusini mwa mkoa wa Idlib na kuwaua watu 12 huku 36 wakijeruhiwa.