Mawakili wampiga mwanafunzi mahakamani India

Image caption Ghasia nje ya mahakama ya mji wa Delhi

Kiongozi mmoja wa wanafunzi kutoka chuo kikuu cha India aliyeshtakiwa kwa kuweka fitna amepigwa katika mahakama moja ya mji wa Delhi na kundi la mawakili.

Kanhaiya Kumar alipigwa na mawakili waliokuwa wakitoa matamshi dhidi yake,ripoti zilisema.

Mahakama imempeleka jela kwa wiki mbili ambapo kesi hiyo itasikizwa tena.

Bwana Kumar alikamatwa baada ya mkutano dhidi ya kunyongwa kwa Mohammed Afzal Guru mwaka 2013 baada ya kupatikana na hatia ya njama ya kutaka kuvamia bunge India mashtaka ambayo aliyakana.

Shambulio hilo lilitekelzwa na wapiganaji wa Kashmir na kuwawacha watu 14 wakiwa wamefariki.

Machafuko hayo yanajiri licha ya mahakama kuu ya India kutoa masharti makali baada ya kikoa chengine cha kusikizwa kwa kesi hiyo kukumbwa na ghasia.

Bwana Kumar alijeruhiwa kutokana na shambulio hilo.