Mkenya miongoni mwa walimu bora duniani

Ayub Mohamud
Image caption Mohamud ni mwalimu wa somo la biashara na lile la dini

Mwalimu mmoja kutoka Kenya ni miongoni mwa walimu wengine kumi waliofuzu fainali ya waliorodheshwa kuwania tuzo ya mwalimu bora katika harakati zake za kukabiliana na itikadi kali.

Ayub Mohamud ni mwalimu wa somo la biashara na lile la dini la IRE katika shule ya upili ya Eastleigh mjini Nairobi.

Tuzo hiyo ya dunia ilioanzishwa na hazina ya fedha ya Verkey,ikiwa ni shirika la hisani la kampuni ya kimataifa ya elimu ya Gems,inayolenga kutafuta habari za mashujaa wanaobadilisha maisha ya vijana.

Image caption Mohamud amekuwa akisaidia kukabiliana na kuenea kwa itikadi kali

Amekuwa akijenga mtandao wa walimu walio na maono kama yake na kutengeza utaratibu unaolenga kukabiliana na itikadi kali.

Tuzo hiyo ilipata maombi kutoka kwa walimu katika mataifa 148.

Mshindi ambaye atatangazwa mwezi Machi ,atapokea dola milioni moja.

Walioorodheshwa ni pamoja na Aqeela Asifi,ambaye anawafunza wakimbizi nchini Pakistan na Hana Al Hroub ambaye alilewa katika kambi moja ya wakimbzi nchini Palestina na ambaye sasa ni mwalimu.

Image caption Mohamud ni mwalimu shule ya upili ya Eastleigh, Nairobi

Mshindi wa tuzo hiyo mwaka jana alikuwa Ancie Atwell kutoka Marekani ambaye alitoa fedha hizo kwa shule yake.

Tuzo hizo zilitolewa katika sherehe iliohudhuriwa na aliyekuwa rais wa Marekani Bill Clinton huku Bill Gates akitoa mchango wake.