Mujuru kuanzisha chama Zimbabwe

Haki miliki ya picha
Image caption Joice Mujuru

Aliyekuwa makamu wa rais nchini Zimbabwe Joice Mujuru amethibitisha kwa chombo cha habari cha AFP kwamba ataanzisha chama chake kitakachopambana na chama tawala cha Zanu-PF kinachoongozwa na Robert Mugabe.

''People First '',alisema Bi Mujuru,akithibitisha jina la chama kipya lakini hakutoa maelezo zaidi.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Robert Mugabe

Mwezi Aprili,BBC iliripoti kwamba Bi Mujuru alitarajiwa kukiongoza chama hicho kufuatia kuondolewa kwake katika chama cha Zanu_PF.

Alishtumiwa na mkewe Mugabe Grace,kwa kupanga kumuondoa rais ,madai aliyoyapinga.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Grace Mugabe

Bi Mujuru alikuwa mshirika wa karibu wa Zanu_PF, zamani na alijulikana kama ''mwaga damu'' wakati wa kupigania uhuru.