Watu 28 wauawa katika mlipuko Uturuki

Shambulio Haki miliki ya picha EPA
Image caption Hakuna kundi lililodai kuhusika

Watu zaidi ya 28 wamefariki baada ya mlipuko mkubwa kutokea katika mji mkuu wa Uturuki, Ankara Jumatano jioni, maafisa wa Uturuki wamesema.

Watu 61 wamejeruhiwa.

Gar lililojaa vilipuzi lililipuliwa mabasi ya jeshi yalipokuwa yakipita, kwa mujibu wa afisi ya gavana wa Ankara.

Mlipuko huo ulitokea karibu na Bunge na makao makuu ya jeshi ya Uturuki.

Naibu waziri mkuu Bekir Bozdag amesema hicho ni “kitendo cha ugaidi”.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mlipuko huo ulisikika kote mjini

Moshi ulitanda angani kutoka eneo hilo na watu walioshuhudia tukio hilo wanasema mlipuko huo ulisikika kote katika mji huo.

Baadhi ya waliofariki na kujeruhiwa walikuwa raia.

Hakuna kundi lililodai kuhusika kufikia sasa.