Shambulio la Uturuki, mhusika hajulikani

Haki miliki ya picha AP
Image caption Ben Rhodes

Serikali ya Marekani bado haijaweza kugundua nani ndiye mhusika mkuu wa shambulio lililotokea mapema wiki hii nchini Uturuki katika mji mkuu wa Ankara,shambulio lililoua watu ishirini na nane.

Akilaani shambulio hilo la bomu lililotegwa kwenye gari, Ben Rhodes, ambaye ni makamu mkuu wa usalama wa Marekani na ambaye pia ni mshauri wa masuala ya usalama,amesema kwamba Marekani itazungumza moja kwa moja na Uturuki kuhusiana na masuala ya usalama ya nchi hiyo.

Viongozi nchi Uturuki wameishutumu Marekani kwa kukiunga mkono chama cha Syria Kurdish na chama cha wafanyakazi wenye asili ya Kurdistan PKK.

Makundi yote hayo mawili yamekana kuhusika katika shambulio hilo,Bwana Rhodes wanauhakika kwamba chama cha YPG kiko kwenye harakati za kupambana na IS ni suala la wazi na kwamba madai ya Uturuki kuishutumu Marekani hayana uzito wowote na kwamba Uturuki ni mshirika muhimu wa Marekani