Soyinka: Wanasiasa walifadhili Boko Haram

Image caption Wole Soyinka

Mmoja wa wawandishi maarufu zaidi duniani mzaliwa wa Nigeria Wole Soyinka amesema kuwa wanasiasa nchini Nigeria ndio walioisaidia kundi la kiislamu la Boko Haram kupata nguvu walioitumia kuua na kujeruhi mamilioni ya watu Kaskazini mwa Nigeria.

Katika mahojiano na runinga ya Channel 4, Soyinka anasema kuwa japo kundi hilo lilipata nguvu na kuwageuka,waowao wanasiasa walikuwana hofu ya kupoteza uungwaji mkono na raia wafuasi wa kundi hilo na hivyo wakaisaidia kundi ambalo baadaye liliwageuka na kuwaua.

Wakati huo mwandishi huyo anasema kundi hilo halikuwa limeanza kampeini yake ya kuua na kuharibu.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Boko Haram inalaumiwa kwa mauaji ya maelfu ya watu

Soyinka ambaye ni mshindi wa tuzo la Nobel aliyasema hayo katika kongamano la wasomi na waandishi katika chuo kikuu cha Oxford kilichokuwa kimeandaa mjadala kuhusu kutolewa au kusalia kwa sanamu ya mkoloni Cecil Rhodes.