Obama asaini vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Obama

Rais Barrack Obama amesaini vikwazo zaidi dhidi ya Korea Kaskazini kuhusiana na mpango wake wa Nuklia, wiki chache tu baada taifa hilo kufanya majaribio ya zana zake za mafasa marefu.

Taifa hilo limekataa kusitisha mpango wake wa nuklia na mswada ulioidhinishwa na bunge la Congress wiki iliyopita.

Vikwazo hivyo vinajaribu kuzuia fedha ambazo Korea Kaskazini ilihitaji ili kuunda zana zaidi za nuklia.

Marekani na Uchina zinashauriana kuhusu azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusiana na vikwazo hivyo vipya.

Uchina imesema kuwa baada ya mikakati hiyo huenda ikasambaratisha uchumi wa Korea Kaskazini.

Vikwazo hivyo ni pamoja na kupiga tanji mali ya mtu yeyote anayefanya biashara inayohusiana na mpango huo wa nuklia na silaha kwa Korea Kaskazini, au kuhusika na ukiukwaji wa haki za kibinadam.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Kim Jong Un wa Korea Kaskazini

Mswada huo pia unaruhusu misaada ya dola milioni hamsini kusaidia utoaji wa misaada ya kibinadamu na kupeperusha matangazo ya Radio nchini Korea Kaskazini.

Hivi majuzi Korea Kaskazini ilifanya majaribio ya zana zake za masafa marefu, kitendo ambacho wakosoaji wanasema lilikuwa jaribio la kiteknolojia la zana za masafa marefu

Runinga ya taifa nchini humo ilitangaza kuwa Korea Kaskazini ilikuwa imefanikiwa kutuma mtambo wake wa Satelite katika anga za juu zaidi.