Mkutano wa kibiashara Afrika waanza Misri

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Abdel Fattak al Sisi

Wajumbe zaidi ya elfu moja wa Afrika, pamoja na viongozi, mawaziri na wafanya biashara, wanahudhuria mkutano nchini Misri, kwa lengo la kuzidisha biashara na uwekezaji katika bara hilo.

Akifungua mkutano huo, Rais wa Misri, Abdel Fattah al-Sisi, alisema lengo moja ni kuonyesha wafanya biashara wa kimataifa, fursa zilizoko Afrika.

Wadadisi wanasema ingawa uchumi wa nchi za Afrika umekuwa ukikua, hata hivyo uchumi wote wa Afrika ni asilimia mbili tu ya uchumi wa dunia.