Uingereza kuamua kuhusu EU

Haki miliki ya picha AFP
Image caption David Cameron

Uingereza itapiga kura ya maoni iwapo itasalia ndani ya muungano wa Ulaya mnamo tarehe 23 mwezi Juni au la,waziri mkuu wa taifa hilo David Cameron ametangaza.

Cameron alitoa tangazo hilo huko Downing Street baada ya kuzungumza na baraza la mawaziri.

Amesema kuwa atafanya kampeni ya kutaka kusalia katika muungano huo uliofanyiwa mabadiliko akisema kuwa kura hiyo itakuwa ya maamuzi muhimu katika maisha ya raia wa Uingereza.

Tayari mawaziri wamejigawanya kuhusu kura hiyo huku kampeni ya kura hiyo ikianza.

Waziri wa maswala ya ndani Theresa May anaongoza orodha ya mawaziri ambao wamesema kuwa watafanya kampeni kusalia katika muungano huo ,lakini waziri wa haki Michael Gove ametia saini ya kuipinga kampeni hiyo.

Wale wanaopigia upatu Uingereza kujiondoa katika muungano huo wanatumai kwamba Meya wa mji wa London Boris Jonhson atajiunga nao,lakini bado hajatangaza msimamo wake.