Volvo kuzindua magari yasiyotumia funguo

Haki miliki ya picha volvo
Image caption Volvo

Kampuni ya kutengeza magari ya Volvo inatarajiwa kujaribu programu moja ya simu nchini Sweden ambayo kampui hiyo inasema huenda ikachukua mahala pa funguo za magari.

Programu hiyo inayotumia BlueTooth inaweza kudhibiti kufuli za milangoni na kuanzisha ama hata kuzima injini ya gari ,lakini kampuni hiyo imeiambia BBC kwamba mikakati zaidi ya kiusalama itatumika ndani ya gari hilo.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Volvo

Programu hiyo pia itawaruhusu wamiliki wengine wa magari kubadilishana ''funguo za kigijitali'' na kupakua funguo hizo kabla ya kupeana magari yao.

Iwapo jaribio hilo litafanikiwa programu hiyo huenda ikazinduliwa mnamo mwaka ujao.

Hatahivyo Volvo imesema kuwa itaendelea kutoa funguo kwa wateja wanaozihitaji,kampuni hiyo imesema.