Jeb Bush ajiondoa mbio za urais Marekani

Jeb Haki miliki ya picha AP
Image caption Jeb Bush hajafanya vyema uchaguzi wa mchujo majimbo matatu ya kwanza

Gavana wa zamani wa Florida Jeb Bush amejiondoa kutoka kwa kinyang’anyiro cha kutafuta mgombea wa urais Marekani kupitia chama cha Republican.

Amejiondoa baada ya kutofanya vyema katika uchaguzi wa mchujo majimbo matatu ya kwanza.

Alimaliza wa nne katika mchujo wa chama hicho jimbo la South Carolina, ambapo tajiri Donald Trump alipata ushindi.

"Leo nasitisha kampeni yangu,” Bw Bush aliambia wafuasi wake.

Alipigiwa upatu kufanya vyema mapema lakini miezi ya karibuni hajakuwa akifanya vyema miezi ya karibuni.

Jeb Bush ni kakake rais wa zamani George W Bush na mwanawe Rais wa zamani George H W Bush.

Katika jimbo la South Carolina, ambapo alitarajia sana kufufua kampeni yake, alimaliza wa nne akishikilia nafasi hiyo pamoja na gavana wa Ohio John Kasich.

Haki miliki ya picha Reuters

"Watu wa Iowa, South Carolina na New Hampshire wamenena, na naheshimu uamuzi wao,” gavana huyo wa zamani amesema, akirejelea kutofana kwake katika majimbo hayo matatu ambayo yamefanya uchaguzi wa mchujo.

"Nimekuwa na maisha mazuri na kwangu, kutumikia umma limekuwa jambo kuu zaidi katika maisha haya maisha yangu,” ameongeza.