Korea Kaskazini yatangaza kamanda mpya wa jeshi

Image caption Aliyekuwa mkuu wa majeshi Ri Yong-gil, alinyongwa baada ya kutuhumiwa kuhusika na ufisadi

Vyombo vya habari nchini Korea Kaskazini vimethibitisha kuwa kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-un amemchagua mkuu mpya wa majeshi.

Aliyekuwa mkuu wa majeshi Ri Yong-gil, alinyongwa baada ya kutuhumiwa kuhusika na ufisadi pamoja na kuunda chama mbadala cha upinzani.

Pyongyang haijasema lolote kuhusiana na madai hayo , lakini mapema leo Jumapili runinga inayomilikiwa na serikali imetangaza kjina la mkuu mpya wa majeshi.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Korea Kaskazini yatangaza kamanda mpya wa jeshi

Ri Myong-su, sasa ndiye kamanda anayesimamia jeshi.

Duru kutoka Korea Kusini wanasema mabadiliko hayo yanathibitisha kuwa makumi ya maafisa wakuu jeshini wameuawa Korea Kaskazini tangu Kim Jong-un atwae madaraka mwaka wa 2011.