Trump aibuka mshindi South Carolina

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Donald Trump

Mgombea kiti wa chama cha Republican katika uchaguzi ujao wa urais nchini Marekani Donald Trump ameshinda kura ya mashinani katika jimbo la Carolina Kusini.

Bwana Trump ambaye awali mwezi huu, alishinda katika jimbo la New Hampshire, amepata kura nyingi huko Carolina Kusini huku wapinzani wake Ted Cruz na Marco Rubio wakimfuatia kwa karibu.

Kutokana na matokeo mabaya ya gavana wa zamani wa Florida, Jeb Bush, kakake aliyekuwa Rais wa Marekani George W. Bush, amejiondoa katika kinyanganyiro hicho.

Haki miliki ya picha AFP y Reuters
Image caption Kutokana na matokeo mabaya ya gavana wa zamani wa Florida, Jeb Bush, kakake aliyekuwa Rais wa Marekani George W. Bush, amejiondoa katika kinyanganyiro hicho.

Awali mgombea kiti hicho kwa chama cha Democrats Bi Hillary Clinton ameibuka mshindi katika kura ya mashinani eneo la Nevada, na kubwaga mpinzani wake Bernie Sanders.