Somalia yataka Kenya ijieleze kuhusu Waziri mkuu

Image caption Waziri mkuu wa Somalia Abdirashid Sharmarke

Serikali ya Somalia imelalamikia vikali hatua ya maafisa wa usafiri wa ndege nchini Kenya kuwanyima ruhusa ujumbe ulioandamana na waziri mkuu wa Somalia ruhusa ya kuabiri ndege ya kwenda Uturuki.

Wajumbe kadhaa waliokuwa na waziri mkuu Abdirashid Sharmarke hawakuwa na ithibati ya usalama na hivyo maafisa wa usalama wa Kenya waliwazuilia kwenye uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta mwishoni mwa juma.

Katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari Somalia inaitaka Kenya, ielezee waziwazi kwanini hilo lilitokea ilihali kunamakubaliano rasmi kati ya serikali hizo mbili kuhusiana na usafiri wa maafisa wakuu serikalini.

Waziri mkuu hata hivyo amekiri kuwa hakuzuiliwa na kuwa waliozuiliwa ni wajumbe walioambatana naye.