Aliyeiba mtoto miaka 18 iliyopita mahakamani

Haki miliki ya picha Eyewitness
Image caption Aliyeiba mtoto miaka 18 iliyopita mahakamani

Kesi dhidi ya mwanamke mmoja wa Cape Town aliyetuhumiwa kumteka nyara mtoto mchanga nchini Afrika Kusini miaka 18 iliyopita, iliyotarajiwa kuanza leo, imeahirishwa.

Mwanahabari wa BBC, Nomsa Maseko mjini Johannesburg amesema , mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 50 aliyekamatwa kwa madai ya utekaji nyara mwezi Februari ameachiliwa kwa dhamana.

Zephany Nurse aliibiwa kutoka kwa kitanda cha mamake siku ya pili tu baada ya kuzaliwa.

Inadaiwa mwanamke huyo alimlea kijana huyo kama mwanaye.

Mtuhumiwa anasemekana kumfanya mamake msichana huyo rafikiye wa karibu alipokuwa bado hospitalini kabla ya kumuiba.

Alimsihi mamake kumsaidia mtoto ili aweze kulala.

Baadaye mfanyikazi wa hospitali hiyo alimuamusha na kumuarifu kuwa mtoto wake ametoweka.

Alipatikana miaka 18 baadaye, baada ya dadake kuwaambia wazazi wake kuna mwanafunzi shuleni mwake wanayefanana naye kama shilingi kwa ya pili.

Uchunguzi wa kina wa vinasaba ulidhihirisha wasichana hao ni ndugu wa baba mmoja na mama mmoja.