Assad awasihi Wasyria warejee nyumbani

Image caption Assad awasihi wasyria warejee nyumbani

Kundi la kislamu la Islamic State limesema lilitekeleza mashambulizi katika mji mkuu wa Syria Damascus na mji wa Homs, ambao uliwauwa watu 140.

Mapema huko Homs watu 57 , wengi wao raia waliuwawa katika mashambulizi mawili ya magari, Kulingana na ripoti za makundi yanayofuatilia habari za nchi hiyo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kundi la kislamu la Islamic State limesema lilitekeleza mashambulizi katika mji mkuu wa Syria Damascus na mji wa Homs

Mashambulizi hayo mawili ya Jumapili yalilenga maeneo yaliozingirwa na waislamu wachache, kama inavyosemekana na kundi la waislamu la Sunni la IS.

Mashambulizo hayo yalitokea baada ya rais Bashar Al – Assad kutoa ripoti kuhusu wakimbizi wa Syria kutoogopa kurudi makao.

Bwana Assad ambaye analaumiwa kwa kuwakandamiza watu wake, aliwaambia waSyria waliokuwa wamehama kutokana vita wasiwe na uoga wowote wa kurejea makwao na kuwa serikali ingewahakikishia usalama.

‘Tunataka watu warudi Syria,’aliambia wanahabari.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Zaidi ya raia 250,000 kutoka Syria wameuwawa katika mashambulizi. Wengine milioni 11 wamehamishwa makwao.

Zaidi ya raia 250,000 kutoka Syria wameuwawa katika mashambulizi.

Wengine milioni 11 wamehamishwa makwao.

Milioni 4 kati yao walihamia nje ya nchi wakijumuisha wale wanaosafiri safari kwenda ulaya.