Dereva wa teksi za Uber mbaroni Michigan

Michigan Haki miliki ya picha EVN
Image caption Ilithibitishwa kuwa Jason Brian Dalton ndia aliekua dereva wa teksi ya Uber

Dereva wa Teksi amekamatwa kwa madai ya vifo vya watu sita katika shambulio la ufyatuaji wa risasi wa kiholela uliotokea katika mji wa Michigan, Kalamazoo.

Jason Brian Dalton, 45, alikamatwa baada ya mashambulio ya sehemu tatu siku ya Jumamosi jioni. Watu wawili akiwemo msichana mwenye umri wa 14 ambaye alipata majeraha mabaya bado wako hospitalini.

Ilithibitishwa kuwa Dalton ndiye aliyekuwa Dereva wa texi ya Uber.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Waendesha mashtaka wanasema Dalton atakabiliwa na shtaka la mauaji makubwa mahakamani

Waendesha mashtaka wanaendelea kuchunguza iwapo alishirikiana na washukiwa wa mashambulio.

Abiria mmoja alisema alipatwa na mshtuko alipokuwa kwenye Texi ya Dalton kabla ya shambulio la kwanza, ambapo aliamua kupigia polisi simu.

Mwendesha mashtaka wa kaunti ya Kalamazoo Jeff Gettings, amesema mshukiwa huyo atakabiliwa na shtaka la muaji la kiwango kikubwa afikapo mahakamani siku ya Jumatatu.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Kampuni ya Uber imesema kuwa mauaji hayo ya kiholela niyakuvunja moyo

Uber imesema imefanya uchunguzi wa maisha ya Dalton na polisi wamethibitisha hakuwa na rekodi ya uhalifu.

Katika taarifa yake, shirika hilo limesema ''limeshushwa na kuvunjika moyo '' kwa mashambulizi hayo.

Polisi wamesema hakuna hata mmoja wa waathiriwa aliekuwa abiria wa mshukiwa.

Dalton alikamatwa majira ya asubuhi siku ya Jumapili baada ya msako wa polisi.